Quantcast
Channel: HOME STIGAS ENTERTAINMENT
Viewing all 303 articles
Browse latest View live

HATIMAYE LULU KUOLEWA HIVI KARIBUNI BAADA YA KUMPATA WAKE SOMA ZAIDI

$
0
0
Hamida Hassan, Mayasa Mariwata na Galdness Mallya
HAYAWIHAYAWI hatimaye yamekua! Siku chache baada ya sexy lady wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kutangaza sifa za mwanaume atakayemchumbia, amejitokeza mtu anayetaka kuchukua jumla na si siri tena, Amani limenyetishiwa.

SIFA ZAKE
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya staa huyo anayekimbiza sokoni na filamu yake ya Foolish Age, mchumba huyo anaitwa Johnson lakini ni maarufu kwa jina la JR na pia ni Mkristo kama ilivyo kwa Lulu.

JR ni mfanyabiashara kigogo wa jijini Dar mwenye ‘mahela’ ya kufa mtu.
Pia mchumba huyo ni bosi wa kampuni kubwa ya uandaaji, usambazaji wa kazi za sanaa Bongo.

ALISHAKWENDA KWA AKINA LULU
“Kwa taarifa yenu, tayari JR anafahamika vizuri kwa akina Lulu kwani alishakwenda kujitambulisha na kuna maneno kwamba ndiye aliyempangia nyumba kubwa, Tegeta jijini Dar.

“Unajua yule jamaa aliona fursa akaitumia. Baada ya Lulu kutoka mahabusu kwa matatizo ya kifo cha mwandani wake, Steven Kanumba ndipo JR akafanya juu chini kumnasa hadi akafanikiwa,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

“Muda siyo mrefu zitasikika cherekochereko za Lulu kuolewa.
“Ukweli ni kwamba hata mama Lulu (Lucresia Karugila) amemkubali yule mchumba kwani ndiye anayemfanya Lulu aonekane kama alivyo kwa sasa.

“Sasa hivi Lulu anaishi kwenye bonge la nyumba kule Tegeta (Dar) na suala la usafiri si ishu. Anabadili tu magari. Kusema kweli kwa sasa bidada mambo yamemwendea vizuri.
“Anachoogopa tu yasitokee kama yale ya Clement wa Wema Sepetu.”

AMANI LASAKA WAHUSIKA
Baada ya kumwagiwa upupu huo, gazeti hili liliwasaka wahusika mmoja baada ya mwingine ili kupata mbivu na mbichi za ishu hiyo.

MAMA LULU
Kwa kuwa ni jambo la kifamilia, gazeti hili lilipozungumza na mama Lulu, Lucresia Karugila alisema si jambo baya kwa mwanaye kuwa na mchumba hivyo anamkubali (huyo mchumba) huku akiweka wazi kuwa hana kipingamizi chochote.

Alipoulizwa jina la mwanaume huyo na kwamba ni kigogo mwenye fedha nyingi, mzazi huyo alitoa ruksa aulizwe Lulu mwenyewe.

“Mimi sina sababu ya kumkataa mwanaume ambaye wamekubaliana na mwanangu, kikubwa ni makubaliano, namkubali,” alisema mama Lulu.


HUYU HAPA LULU
Kwa upande wake Lulu mambo yalikuwa hivi;
Amani: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Poa, naongea na nani?
Amani: (akatajiwa jina la mwandishi) kwanza hongera kwa kupata mchumba.
Lulu: Nani kawaambia?

Amani: Kwa kazi yetu hii hatushindwi kujua. Je, ni kweli umepata mchumba?
Lulu: Ndiyo lakini nisingependa sana kulizungumzia hilo.
Amani: Anaitwa nani?
Lulu: Siwezi kumtaja leo (Jumanne iliyopita). Nitawatajia tu ninyi subirini. Itakuwa surprise (mshangao), siku si nyingi nitamuanika.

Amani: Je, ni kweli ni maarufu kwa jina la JR? Au wewe tutajie hata jina la mwanzo tu.
Lulu: Nimeshasema jamani nitawatajia kwani ninyi mna haraka gani?
Amani: Je, ni kweli ni mmiliki wa kampuni ya burudani? (anatajiwa kampuni).
Lulu: Hayo yote yatafahamika kwenye utambulisho. Naomba niishie hapo ‘coz’ sina cha zaidi kuhusu ishu hiyo jamani subirini siku si nyingi.


MAMA KANUMBA
Baada ya kujiridhisha kuwa sasa Lulu ana mchumba rasmi, ‘kijumbe’ wetu alimfikishia taarifa aliyekuwa mama mkwe wa staa huyo wakati akiwa na Kanumba, mama Kanumba, Flora Mtegoa ili naye atie neno.

Mama Kanumba hakuwa na kipingamizi juu ya suala hilo zaidi ya kuchekelea huku akiweka wazi kuwa Lulu kwa sasa anaweza kuolewa.
“Mimi sina tatizo kabisa, namjua. Lulu anaweza kuolewa na nimempa baraka zote,” alisema mama Kanumba ambaye kwa sasa ni shosti mkubwa wa mama Lulu.

JR SASA
Hata hivyo, gazeti hili halikuishia hapo kwani lilisaka namba ya simu ya kiganjani ya mwanaume huyo ambapo ilipopatikana, alipigiwa, mambo yakawa hivi:
Amani: Habari yako mkuu JR?
JR: Safi, nikusaidie nini?

Amani: Mimi…(akatajiwa jina la mwandishi na kampuni) wewe ndiye JR mmiliki wa kampuni ya…(anatajiwa jina la kampuni).
JR: Kwanza mimi siyo JR ni GR. Huyo JR ni mdogo wangu.
Amani: Mbona sisi tumetajiwa JR ambaye anamiliki kampuni ya...(anatajiwa tena jina la kampuni).
JR: Oke, ndiyo mimi nikusaidie nini?

Amani: Taarifa tulizonazo ni kwamba una uhusiano na Lulu? Yaani wewe ndiye mchumba wake?
JR: Ndiyo, sitaki maswali (tusi na kukata simu).  
Tangu kitokee kifo cha Kanumba ambaye alikuwa na uhusiano wa siri na Lulu, bidada huyo hajawahi kuwa na mwanaume hadi huyo mchumba aliyejitokeza.

YADAIWA MSANII WA BONGO MOVIE JOHARI YUPO HOI AMELAZWA HIVYO NI VYEMA KUMUOMBEA (GET WELL SOON)

$
0
0
http://3.bp.blogspot.com/-VA8jHBZIXqU/UWZgEtwuHLI/AAAAAAAAeZM/ijbeWaHQv50/s1600/JOHARI.jpg 

Mwana Dada na mwigizaji mkongwe Blandina Chagula maarufu Johari ni mgonjwa na amelazwa katika moja ya hospitali maarufu hapa jijini.

http://bongocelebrity.files.wordpress.com/2008/06/joharibc.jpg%3Fw%3D591%26h%3D392

 
Kwa mujibu wa blogu ya mwigizaji Deogratious Shija, ndugu wa karibu wa Johari ameshindwa kuweka wazi ni hospitali gani ambayo Johari amelazwa na kusema kuwa wanashindwa kusema mahali alipolazwa Johari kutokana na usumbufu wa waandishi wa habari " kwakweli Johari anaumwa sana na tunaomba dua zenu tu" Alisema ndugu huyo wa johari. Jamani tumumkumbuke katika dua muigizaji huyu na wagonjwa wengine wote mahospitalini. Ameni

HIVI NDIVYO KOLETA ALIVYOTILILIKA KUHUSIANA NA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE SOMA ZAIDI

$
0
0
BISHOSTI anayeuza nyago kwenye filamu za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ amefunguka kuwa analaani mastaa wanaokubali kutumiwa kimapenzi kinyume na maumbile akidai kuwa wapo ambao wamekuwa wakifanya kitendo hicho kwa tamaa ya pesa.


 
Coletha Raymond ‘Koleta’.
Akistorisha na Paparazi wetu, Koleta alisema anachukizwa na tabia hiyo kwani ni uchafu na kujidhalilisha kulikopitiliza.

“Wanaume siku hizi ni matapeli sana, wengi wanataka kuwatumia wanawake kinyume na maumbile hivyo wasanii wa kike tuwe macho. Alishawahi kunitokea mwanaume mwenye heshima zake, alinipigia simu na kuniambia licha ya kuwa na mke kuna vitu anavikosa.

 

Nilipomuuliza ni vitu gani akaniambia anataka anitumie kinyume na maumbile na nichague zawadi isiyopungua milioni tano aniletee, nikakataa na kumwambia sifanyi biashara hiyo, ukweli mimi nakemea na ninawachukia sana wanaofanya mchezo huo,” alisema Koleta.

HUYU NDO MREMBO ANAYEDAIWA KUTOKA NA MKALI DIAMOND KWA SASA MTAZAME HAPA

$
0
0
 
Ama kweli wadada wa mjini wana mambo sana, wenyewe wanasema kua mjini shule kijijini kilimo. Sasa huku kuja kwa mitandao ya jamii kumeibua makubwa ambayo tulikua hatuyajui. Mwanzo Facebook ilikua ndo kila kitu kwa umbea wote wa town unaupata kule ila kwa sasa mambo yamebadilika kabisa, Insta ndo habari ya mjini. Kila kitu utakipata Insta hadi madalali lol.
Sasa habari tulizozipata kutoka huko huko insta ni kua baada ya Raisi wa wasafi bwana Diamond au Halima Kimwana anavyopenda kumwita Chibu Dangote kutemana na mwanadada DvjPenny na tetesi kusema kua Diamond wamerudiana na wema hili tulilolinasa laweza kuwashangaza wengi sana.

Habari zilizotafutwa na mdakuzi wetu kupitia mtandao mmoja maarufu zinasema kua Bwana Diamond ana mtoto mpyaaa tena mkali ile mbaya. Katika pitapita yetu Insta tukakutana na post ya mtu mmoja hivi ambaye kila kukicha yeye ni kumtetea aliyekua X wa Diamond mwanadada Penny. Post hiyo iliandikwa 
"Uwiiiiii chaggabarbie aijasimama Bado hapo au nayo kibamia kwako ivi nimuulize diamondplatnum nae anayo kama hiyo nn eti wemasepetu vjpenny04 mana mnatoana macho kwa mtoto wa tandale sasaivi nasikia anapumzika kwa hamisa mobeto wanafata hii Kitu Kina dada tuambizane na dai nae anayo nini kama anayo ukitoka kwa hamisa nenda zamu chagga Basi uwiiiiii chaga una balaa ww Kitu na box ndomambo yako chagga be like keep calm its just a big di**" 

Sifa kubwa ya mwenye hiyo akaunti ni kumtetea sana Penny na nahisi atakua ni mtu wake wa karibu kwani kuna vitu vingine anaandika ni vigumu kwa mtu ambaye si wa karibu na Penny kuvijua. Waswahili wanasema kua lisemwalo lipo na kama halipo basi laja, Je ni kweli Bwana Diamond anatoka na mtoto mzuri Hamisa????? Swali linabaki hapo???
Lakini kama utakua mfatiliaji mzuri wa mastory haya utakumbuka kua karibu mademu wote waliotembea na Diamond na baadae kujulikana ilianza kama tetesi hivi hivi, mfano mzuri ni Wema, Yule aliyekua demu wa Mr Blue, Penny, Jokate na wengine ambao ni ngumu kuwataja.

Kwa wale msiomjua Hamisa ni nani, ngoja niwape profile yake kwa ufupi tu. Hamisa ni Model. Umaarufu wake umeongezeka sana siku za hivi karibuni kwani kuna makampuni mengi yanamtafuta kufanya matangazo nae kutokana na uzuri alionao. Kwa wale mlibahatika kuliona Jarida la Pulse Kenya mwezi huu mwanadada Hamisa ndo alipamba ukurasa wa mbele.

Kama ni kweli Bwana Diamond kaamua kujituliza kwa Hamisa itakua poa coz mtoto kasimama kila idara, Unaweza tazama picha kibao za mwanadada huyu mkali Hamisa zilizokusanywa kwa hisani ya bongoclan hapa chini....

MSANII JACKLINE DUSTAN ATILILIKA ADAI ANAJILENGESHA KWA WAZUNGU ILI APATE MIMBA SOMA UJUE ZAIDI

$
0
0
Mwanadada Jacqueline Dustan ambaye ni msanii wa filamu aliyeibukia kwenye Shindano la Maisha Plus season II, ameonekana kung’ang’ania kuzaa na Mzungu kufuatia maelezo yake kwamba harudi Bongo mpaka atundikwe mimba na mtasha.
Jacqueline Dustan.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu akiwa nchini Thailand, Jack alisema uwepo wake nchini humo kwa muda mrefu anajilengesha kwa mwanaume wa Kizungu ambaye atampenda na ikiwezekana amzalie mtoto.
“Kwa kweli nitarudi Bongo endapo tu nitapata mtoto mmoja wa kitasha, sasa niko bize kutafuta mchumba ambaye ni salama kwangu ili niweze kupata naye mtoto mmoja tu,” alisema Jack.
 
Ni takriban mwezi wa sita sasa msanii huyo yuko nchini humo huku anachokifanya kikiwa hakijulikani licha ya kuwepo kwa madai kuwa, wasanii wengi wanaokwenda huko wanajiuza.

GPL

BAADA TU YA LULU KUTANGAZA KUOLEWA SINTA AJA NA USHAURI MZITO KWAKE ENDELEAAA

$
0
0
http://api.ning.com/files/mzLbifxKbCRieysE6S9nVzFnJ4Iym44hEJpXNHJhpFg44Rvs*yBSWe0tTpuBBjLcs0hDwgKEMxa4eCIf8IYtdDUDjCkygVPx/lulu.jpg%3Fwidth%3D600 

Ninakutakia kila la kheri ila kuwa muangalifu na wanaume maana kuna wa aina mbili masikini na matajiri, wale masikini watakupenda kwa dhati wakiwa hawana ila siku wakipata utawajua wao nani, ama uongo wadau?
Na wale matajiri watajua umependea pesa zao na hata kama umempenda kwa dhati mambo ya manyanyaso na nk yatahusika, esp matajiri watakuhonga kila kitu make sure hata akikununulia kijiko kiwe katika jina lako Elizabeth Michael.

http://3.bp.blogspot.com/-d3kNFV2zfNk/T4Lsrvh5H9I/AAAAAAABXzY/dwT8CTSCS0o/s640/263153_145107392232890_100002008907798_288792_3039724_n.JPG

All the best maana sasa umekuwa yaliyopita si ndwele tugange yajayo, one more thing, mfiche mtarajiwa wako we anza kumtangaza anaitwa J haaa kuna makubimbiri yanan'gaa macho kazi yao kusubiri kutongozwa halafu yalivyokuwa mahayawani yenyewe yanakuja kwa nia moja tu ya kuharibu na kusepa so TAKE CARE.... 

USISAHAU KUPITIA KURASA ZA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARY 24 2014 HAPA

$
0
0
.


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

JOHARI ANENA HAYA " .“Siwezi kuzungumza vizuri, sauti yangu iko chini sana... nahisi kama inakauka...." TUMUOMBEE NDUGU WATANZANIA

$
0
0

MASKINI JOHARI....“Siwezi kuzungumza vizuri, sauti yangu iko chini sana... nahisi kama inakauka...."

MASKINI! Ndiyo neno linaloweza kumtoka mtu yeyote mwenye mapenzi mema na staa wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ambaye kwa sasa afya yake si ya kuridhisha, Ijumaa lina kila kitu.
Blandina Chagula ‘Johari’.
Johari ni mgonjwa kwa zaidi ya siku tano sasa akiwa mtu wa kwenda hospitali mara kwa mara kwa ajili ya kuendelea na matibabu.

TAARIFA ZA AWALI
Shostito wa karibu na staa huyo alipiga simu chumba cha habari cha gazeti hili, wiki iliyopita akieleza kwamba Johari ni mgonjwa na amekuwa mtu wa kupumzika ndani.

Rafiki huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema: “Najua mtakuwa hamna hii habari, lakini kiukweli Johari anaumwa, jana (Jumanne iliyopita) nilikwenda kwake, hali niliyomkuta nayo kwa kweli nilimhurumia, yawezekana pia ile ishu yake na Ray inamchanganya, ukimuona amepungua, siyo yule unayemjua.”

Blandina Chagula ‘Johari’.
JOHARI ATAFUTWA
Katika kutaka kujiridhisha, mmoja wa wahariri wa Global Publishers, alimvutia waya Johari Jumanne iliyopita, ambapo alipokea na kuzungumza kwa shida huku sauti ikiwa chini sana.

“Siwezi kuzungumza vizuri, sauti yangu iko chini sana... nahisi kama inakauka. Naumwa sana. Nina fluu,” alisema Johari.
Baada ya mazungumzo hayo, gazeti hili lilipata uhakika kuwa ni kweli Johari ni mgonjwa lakini hakuwa ‘siriazi’ kivile, likachukulia poa. 

HALI YABADILIKA
Siku mbili baadaye, chanzo chetu kilekile cha awali kilipiga tena simu na kutoa taarifa kuwa hali ya Johari ilibadilika ghafla na kwamba alifikishwa hospitalini.
Hata hivyo, alipoulizwa ni hospitali gani amelazwa, alisema hana uhakika lakini alisikia kama amepelekwa AAR ya Sinza. Simu ya Johari ilipopigwa, haikupatikana achilia mbali marafiki zake wa karibu. 

MAPAPARAZI HOSPITALINI
Timu yetu ilifunga safari hadi Hospitali ya AAR (Sinza) na ile nyingine ya Posta na kujaribu kudodosa kama alifikishwa hospitalini hapo, likaambulia patupu. 

STEVE NYERERE AANZA KAZI
Katika kuonyesha kuwa mwenyekiti mpya wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ amedhamiria kuweka umoja na ushirikiano kwa wasanii walio kwenye klabu hiyo kwenye shida na raha, ndiye aliyemtoa Johari hospitalini.

Steve Nyerere aliweka picha kwenye ukurasa wake wa Instergram inayomwonesha Johari akiwa katika hali ya kuugua, huku mkononi mwake akiwa na plasta iliyoonyesha kuwa alitundikiwa drip na kuandika: “Johari haya ndiyo maisha, usijali utapona.” 
MAPAPARAZI NYUMBANI KWA JOHARI
Juzi Jumatano, timu ya waandishi wetu ilifunga safari hadi nyumbani kwa Johari, Ubungo – External, Dar ili kujua hali yake.
Hatua chache kabla ya kufika nyumbani kwake, gazeti hili lilimpigia simu, lakini hakupokea badala yake alilitumia ujumbe mfupi uliosema: “Siwezi kuongea, naomba unitumie meseji, naumwa sana na fluu, naamini nitapona. Nitakutafuta.”
Ijumaa: Nipo na karibu na kwako, nakuja kukuona.
Johari: Sipo nyumbani, nipo hospitalini.
Ijumaa: Hospitali gani?
Johari: AAR. 

UHAKIKA
Pamoja na majibu ya Johari, bado gazeti hili lilitaka kujiridhisha zaidi, halikuishia njiani, lilifika hadi nyumbani kwake ambapo lilipokelewa na kijana wa kiume aliyekataa kutaja jina lake lakini alijitambulisha kama mdogo wake na Johari.

Alipoulizwa kuhusu Johari, haraka alisema: “Dada anaumwa, amekwenda hospitali. Kwa nini msiwasiliane naye kwenye simu?”

INASIKITISHA MWANAFUNZI CHUO KIKUU IFM AKUTWA AMEKUFA CHUMBA CHA KUPUMZIKIA

$
0
0

 
Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ibrahim Jackson (24), amekutwa akiwa amekufa katika chumba cha kupumzikia kilichopo chuoni hapo bila mwili wake kuwa najeraha lolote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema tukio hilo lilitokea saa 11:30 juzi jioni katika chumba namba 118 jengo namba D kilichopo mtaa wa Shaban Robert.
NIPASHE lilifika IFM na kuzungumza na Mshauri wa Wanafunzi, Emmanuel Mushi, ambaye alisema kuwa marehemu alikuwa anasomea Shahada ya Usimamizi wa Kodi akiwamwaka wa pili.

Alisema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM.
Alisema juzi jioni marehemu aliomba funguo kwa ajili ya kwenda kupumzika katika chumba kinachotumiwa kulala nawanafunzi kutoka nje ya nchi pindi wanapofika chuoni hapo kwa ajili yamasomo.

“Nyaraka zake zinaonyesha marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu, hata kabla hajajiunga na chuohiki, kwa hapa chuoni ugonjwa huo ulikuwa unamtokea mara kwa mara,” alisema Mushi.

Aliongeza kuwa mara baada ya kupewa funguo alikwenda kupumzika katika chumba hicho na baadaye alikutwa amefariki huku mwili wake ukiwa umelala kitandani.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa katika kituo cha polisi napolisi walifika katika chumba hicho na kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Mushi alisema wamewasiliana na wazazi wake waliopo wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya na taratibu za kuusafirisha mwili huo zitafanyika leo.

Mmoja wa marafiki wa karibu wa marehemu, Peter Alphonce, aliliambia NIPASHE kuwa alikuwa na marehemu siku moja kabla ya kifo chake wakicheza mpira na walimaliza kucheza vizuri na kuagana kuelekea hosteli.

“Nilikuwa naye jana (juzi) tukicheza mpira, hadi saa kumi tulipomaliza aliniaga na kuelekea katika MachavaHostel ndiko anakolala,” alisema Alphonce.
 
NIPASHE.

MWANAMUZIKI NA MUIGIZAJI SHILOLE APEWA MAFUNZO YA DINI ASHAURIWA KUACHANA NA MAMBO YA KUCHEZA NUSU UCHI

$
0
0
STAA wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa jukwaani akifanya shoo ya kidunia na kupewa darasa la wokovu.
 Zuwena Mohamed ‘Shilole’(kulia) na Mchungaji.
Tukio hilo lililowagusa wengi, lilitokea juzikati katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar ambapo mchungaji huyo ambaye hakupenda kujitambulisha jina lake, alifuatilia shoo ya Shilole kisha akamwita kumpa darasa la wokovu.
Akizungumzia tukio hilo kwa kinasa sauti cha Weekly Exlusive Star, Shilole aliweka plain kuwa, mchungaji huyo aliguswa na namna ambavyo watu wengi walikuwa wakifuatilia shoo yake, akaona anaweza kuwabadilisha wengi waliopotea kupitia wokovu.
“Aisee ilikuwa noma, nilipoona ananiita nilishtuka kidogo. Mbaya zaidi aliniambia anataka tupige picha pamoja, ndipo alipoanza kunipa darasa la wokovu. 
“Alinitaka nibadilike kimavazi, pia nisimsahau Mungu katika maisha yangu yote na alimalizia kwa kunitaka niende kanisani kwake ili ikwezekana nitumie uimbaji wangu kuwabadilisha wengi waweze kumtumaini Bwana,” alisema Shilole staa wa wimbo Nakomaa na Jiji. 
Hata hivyo, katika mazungumzo hayo, Shilole alionekana kuguswa na maneno ya mchungaji huyo na kusema yamemkumbusha suala la kumkumbuka Mungu kila wakati katika kazi za mikono yake. 
Akasema kwa kuzingatia hilo, sehemu ya mapato yake atakuwa akiyatumia katika kutoa sadaka husan kwa watu wasiojiweza ili kutimiza amri ya Mungu.
“Ni wakati wa kubadilika, huu muziki tunafanya  upo na utaendelea kuwepo lakini jambo la muhimu sana ni kumuabudu Mungu katika siku zote za maisha yetu ya hapa duniani,” alisema Shilole.

VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI, JANUARY 25

$
0
0
...
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA MWANADADA HAMISA BAADA YA STORY KUZAGAA KUWA NDIYE DEMU MPYA WA MKALI DIAMOND

UJUE UKWELI WA KASHFA YA KUSAGANA KATI YA IRENE UWOYA NA MARIAM SOMA ZAIDI

$
0
0
http://filamucentral.co.tz/wp-content/uploads/2013/04/Mariam-Ismail-3-cut.jpg
 
Mariam Ismail
Mastaa wa filamu nchini Mariam Ismail na Irene Uwoya wanadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi(usagaji) na kudaiwa kuishi pamoja kabisa. wiki kadhaa nyuma muigizaji mmoja chipukizi anayekuja juu kwa kasi aliutonya mtandao huu kwa kusema " Mariam Ismail na Uwoya wanasagana tena wanaishi pamoja kabisa, fuatilieni mtajua". 

Baada ya habari hizo ilibidi Swahiliworldplanet kuwatafuta mastaa hao, wa kwanza kutafutwa akiwa Irene Uwoya lakini namba yake ya simu kwa takribani wiki 2 ilikuwa haipatikani na hata jana alipotumiwa ujumbe kupitia namba yake nyingine hakujibu.

Baada ya hapo ilibidi kumtafuta Mariam Ismail ambaye wamecheza filamu nyingi na Irene Uwoya kama vile Sobbing Sound, Omega Confusion, The Return Of Omega na Apple, Hata hivyo Mariam anafanya vizuri katika filamu alionekana kuwa busy na kuchelewa kujibu ujumbe wa madai ya kusagana na Uwoya lakini jana star huyo aliyejipatia umaarufu kwa kuuvaa vizuri uhusika katika filamu zake alitoa ushirikiano mzuri kwa kujibu madai hayo akidai sio kweli ila yeye na Uwoya ni marafiki wa karibu sana na wanasaidiana katika shida na raha ndiyo maana baadhi ya watu wameshaanza kusema vibaya...

http://1.bp.blogspot.com/_EIl8I8kB83U/TFid9q0AT7I/AAAAAAAAGks/jvleWE372GE/s1600/DSCN3335.JPG%3Fwidth%3D450
 
"Nadhani mimi ndio mtu wa kwanza kupiga vita upumbavu kama huo... mimi ni mwanamke ambae nimeumbwa kikamilifu.. sina kasoro yoyote ya kunifanya niwe na mwanamke mwenzangu....hao wanaofanya upumbavu huo nadhani wana vijikasoro kwenye mili yao.... Irene Uwoya ni rafiki yangu sana tena urafiki wetu sio wa leo wala kesho... ni marafiki wa kushibana kabisa... nikoseapo huwa ananikosoa na yeye akoseapo huwa namkosoa....sometimes huwa tunagombana na kupatana vitu ambavyo ni vya kawaida katika maisha." alisema Mariam ambaye hajawahi kukumbwa na skendo yoyote ile kabla. 

http://laivu.com/lindiyetu/files/2012/12/irene.jpg

Mariam ambaye kipaji chake cha filamu hujionyesha waziwazi alimalizia kwa kusema "Irene ananiheshimu sana na mimi humuheshimu sana Irene, imefikia hatua ya mimi na yeye tukakaa chini na kupanga tuishi wote kitu ambacho sioni tatizo na hilo. Ingekua ni chumba kimoja hapo sawa... lakini ni nyumba kubwa yenye kujitosheleza...kila mtu na room yake...tunaishi kwa amani na kwa kushirikiana penye tatizo hulitatua wenyewe bila kumshirikisha mtu.

MSANII BONGO MUVIE ANYWA SUMU KISA KIKIDAIWA NI MAPENZI

$
0
0
Msanii chipukizi wa filamu wa Kundi la Mwamba Arts, Mariam Glant.
MSANII chipukizi wa filamu wa Kundi la Mwamba Arts, Mariam Glant (20) amenusurika kifo baada ya kunywa sumu kisa kikidaiwa kuwa ni penzi la kijana aliyejifanya mdogo wa Kanumba anayejulikana kwa jina moja la Chief.
Akizungumza na paparazi wetu sosi wa karibu na msanii huyo alisema siku ya tukio, Mariam alikuwa nyumbani kwa rafiki yake wa kike maeneo ya Mbezi Mwisho, jijini Dar ambapo rafiki yake huyo alitoka kidogo na kumuacha peke yake nyumbani hapo. 
Sosi huyo alisema baada ya muda mfupi alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa Mariam ukisema ‘mimi ndiyo nakufa hivyo nimekunywa sumu.’ 
Baada ya rafiki huyo kupata ujumbe huo, alirudi nyumbani haraka na kumkuta Mariamu akiwa amezimia huku akitokwa na mapovu mdomoni ambapo kwa kushirikiana na wasamaria wema walimchukua na kumkimbiza kituo cha polisi kuchukua PF3 na kumpeleka hospitali ya tumbi ambapo alipatiwa matibabu.
Akielezea kwa uchungu baada ya kupata ahueni, Mariam alisema yeye na mpenzi wake huyo waligombana siku chache kabla hajachukua uamuzi wa kunywa sum

“Sababu kubwa iliyonifanya ninywe sumu ni huyo mwanaume kwa sababu kwanza alinidanganya yeye ni mdogo wake Kanumba na nikiwa naye kimapenzi atanitoa kisanaa na nitakuwa maarufu lakini baada ya kuingia kwenye uhusiano hakunisaidia chochote zaidi nilikuja kugundua kwamba hana hata undugu na Kanumba tukagombana,” alisema Mariam aliyeng’ara katika sinema za Mwanamipango Comedi, Gods Kingdom na M23

BALAA MREMBO ANUSURIKA KUFA KISA WIZI WA SIMU

$
0
0
MREMBO mmoja mkazi wa Mabibo Makutano jijini Dar es Salaam (jina lake halikupatikana) mwishoni mwa wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya kuvamiwa na kudundwa baada ya kudaiwa kukwapua simu ya mwanaume na kuificha sehemu zake za siri.


Mrembo akiwa chini baada ya kuchezea kichapo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, awali mrembo huyo alikuwa akila bata na mwanaume aitwaye Hashim kwenye Baa ya Jassun Inn iliyopo maeneo ya Mabibo huku mwanaume huyo akiwa ametandaza simu zake za kisasa juu ya meza.

Imedaiwa kuwa wakati wakiendelea kuponda raha, Hashim alikwenda msalani kwa lengo la kujisaidia na kuacha simu zake mezani, aliporudi hakumkuta mrembo aliyekuwa akiponda naye raha na simu yake moja haikuwepo.


...Akiwa amewekwa mtu kati na wananchi.
“Jasho lilimtoka Hashim na kuwauliza watu waliokaa jirani alikoelekea mrembo huyo,” alisema shuhuda mmojawapo wa tukio hilo na kubainisha kwamba msamaria mwema mmoja alimweleza Hashim mwelekeo wa mrembo huyo.

Bila kuchelewa Hashim aliwakusanya wapambe wake na kuanza kumtafuta mrembo huyo na wakamnasa mita kama 150 kutoka Baa ya Jassun na kumuuliza kuhusu simu iliyokuwa mezani lakini alileta ubishi.

Walijitahidi sana kumbembeleza ili aitoe simu kwa hiyari yake lakini alikataa, ndipo Hashim na wapambe wakamwanzishia songombingo la nguvu na kufikia kumvua nguo hadharani na simu ikakutwa kwenye nguo yake ya ndani,” shuhuda wetu alisema.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, hadi kufikia kupatikana kwa simu hiyo, mrembo huyo alikuwa hoi kutokana na vurugu aliyofanyiwa na wapambe wa Hashim ambao walipoipata simu walimvisha nguo pamoja na wigi lake lililokuwa limemvuka.

VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO ALHAMISI YA JANUARY 30

$
0
0
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

TAZAMA SHILOLE ANASWA NA MTASHA AMBAYE INADAIWA NI MCHUMBA WAKE TILILIKA NAYO

$
0
0
KWA mara ya kwanza msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa akiwa na mwanaume wa Kizungu anayedaiwa kuwa ndiye mchumba wake.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mchumba wake.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, safari za mara kwa mara za Shilole nchini Uingereza zimekuwa zikisababishwa na mchumba huyo wa Kizungu ambaye huwa anamuita kufurahia penzi lao pamoja na kumtafutia shoo mbalimbali. 
“Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba wa Kizungu na walikutana kwenye shoo ya mara ya kwanza aliyoenda kufanya nchini Uingereza na hivi karibuni ataenda tena na amealikwa na huyo mchumba wake,” kilisema chanzo hicho. 
Gazeti hili limekuwa la kwanza kunasa picha kadhaa za Shilole akiwa katika mapozi tofauti ya kimahaba na Mzungu huyo. 
Baada ya chanzo hicho kumwaga ‘upupu’ huo, mapaparazi wetu walimtafuta Shilole ili aweze kufunguka ambapo bila kuumauma maneno, alikiri kuwa amepata mchumba huyo aliyemtambulisha kwa jina la Ankar. 
Akizidi kumwaga data za boifrendi wake huyo, Shilole alisema awali walikutana kwenye moja ya shoo zake nchini humo ndipo urafiki ulipoota mizizi na kufikia hatua ya kuwa wapenzi. 
“Kweli nina mchumba Mzungu ambaye ni raia wa Uingereza, nilipokuwa napataka nimefika, sipindui tena. Unajua muziki wangu na mauno yangu yanawavutia sana watu, siku ya kwanza aliniona kwenye shoo akanipenda ndipo tukaanzisha urafiki.

“Hivi karibuni nina safari ya kwenda nchini humo kwa mwaliko maalum alionipa, nitaenda peke yangu kwani safari nyingine zote zilizopita nilikuwa naenda na watu,” alisema Shilole. 

MAMA WA MREMBO WEMA MTAA KWA MTAA KUMTAFUTA BINTI YAKE WEMA SOMA ZAIDI

$
0
0
HABARI mpya! Mama wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu anadaiwa kuingia rasmi mitaani akiwasaka wapenzi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Wema, chanzo cha uhakika kimesema na Amani.

Wema na Diamond wakiwa katika pozi la kimahaba.
Kwa mujibu wa chanzo hicho makini, mama Wema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kusikia taarifa kutoka kwa watu kwamba, Diamond amekuwa akisambaza maneno mitaani kuwa haogopi vitisho vya mwanamke huyo kufuatia hatua yake ya kumrudia binti yake.

ILIKUWAJE KWANI?
Hivi karibuni, mama Wema alizungumza na gazeti tumbo moja la hili, Ijumaa Wikienda linalotolewa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kila siku ya Jumatatu na kusema kitendo cha Diamond kumrudia bintiye hakubaliani nacho.
Aliongeza kuwa, kufuatia hatua hiyo iko siku ataingia mtaani kumsaka Diamond na popote pale atakapomnasa, atamkata na panga.

Mama Wema, Mariam Sepetu anayewasaka wapenzi hao.
TURUDI KWA CHANZO
“Jamani si mnakumbuka juzikati mama Wema alisema atamsaka Diamond? Sasa amesikia Diamond anatangaza mitaani kwamba, hatishiki na tamko la mama mkwe wake huyo na watakapokutana watajua nani zaidi.
“Hivi ninavyosema, mama Wema ameingia mtaani kuwasaka. Lengo lake awakute wote wawili ili awaanzishie timbwili la kufa mtu.
“Tangu Ijumaa iliyopita, kila siku anatoka kwenda mitaani kuwasaka, naamini siku akiwakuta pamoja kweli itakuwa vita kubwa,” kilisema chanzo chetu.

Gari la Wema na la Diamond yakiwa yameegeshwa nyumbani kwa Wema.
KWA NINI ASIENDE NYUMBANI?
Chanzo kilipoulizwa kama kweli mama Wema amepania kuwanasa wawili hao, kwa nini asiwafuate nyumbani kwa binti yake, Kijitonyama, Dar ambako wanapika na kupakua, kilijibu:
“Ameweka mtego wake pale, bahati mbaya sana Diamond naye anaishi kwa machale. Kuna siku anakwenda kulala kuna siku haendi. Huenda na yeye (Diamond) ameweka watu wake ndani kwa Wema wa kumpelelezea kama mama Wema atakwenda au ana dalili za kwenda.”
Chanzo kikaendelea: “Siku hizi Diamond anaweza kwenda kwa Wema, akaacha gari lake na kutoka na la Wema na kurudi kwake usiku sana.”

Paparazi wa GPL akiwa nyumbani kwa Diamond.
AMANI LAWASAKA WAHUSIKA
Baada ya kuzinyaka nyeti hizo, Amani liliamua kuutafuta ukweli ambapo Jumanne iliyopita lilimsaka mama Wema kwa njia ya simu lakini iliita bila kupokelewa.
Amani lilitumia simu zake mbili kumpigia mwanamke huyo.
Baada ya dakika tano, mama huyo mwenye ‘machungu’ na mwanaume yeyote anayemchezea bintiye alituma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) akisema: Nipo msibani tuma sms. Pia akatuma sms kwenye simu ya pili akisema: Nipo msibani, ulikuwa unasemaje?
Amani lilimtumia madai yote kuhusu yeye kuanza kuwatafuta Wema na Diamond, pia likamjulisha kwamba kama anawatafuta kweli, muda huo, wawili hao walikuwa wapo chumbani kwa Wema hawajaamka.
Hata hivyo, mama Wema hakujibu meseji yoyote kati ya hizo mbili hali iliyotafsiriwa na Amani kuwa, uchungu wa msiba ulimuondolea uwezo wa mawasiliano.

Paparazi wa GPL akiongea na mlinzi wa Wema nyumbani kwake.
NYUMBANI KWA DIAMOND
Mapaparazi wetu walitia timu nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori na kukutana na mtu mmoja aliyedai ni mjomba wa staa huyo ambaye alidai Diamond Platnumz alitoka asubuhi na mama yake, Sanura Kassim kwenda Tegeta, Dar.
NYUMBANI KWA WEMA
Baada ya kutoka nyumbani kwa Diamond huku wakiamini Mbongo Fleva huyo kaenda Tegeta kama alivyosema mjomba mtu, mapaparazi walikwenda nyumbani kwa Wema.
Baada ya kugonga geti kwa dakika moja, alitokea mlinzi na mambo yalikuwa kama ifuatavyo;
Paparazi: Mambo?

Wema.

HATIMAYE SINTAH AFUNGUKA NA KUMPONDA NAIMA MTOTO WA KIARABU ALIYERITHI PENZI LA WEMA KWA KIGOGO WA SERIKALINI

$
0
0
Naima aliechukua nafasi ya madam
yaani ndipo nina amini wanawake
mwalimu wetu ni kipofu
upo na mwanaume less than 2 months
 unajichora hivi

Naima aliechukua nafasi ya madam

Kila siku nasema bora marafiki zangu wawe mapaka na mambwa, sasa so called kigogo wa madam amekaa hapo juu sasa, sasa huyu dada jamani daah yaani mtu umemjua hata miezi miwili bado umeshajisexisha kiasi hiki na kuchora tattoo, kweli wanawake tunajishangaza wenyewe, sasa yeye anaona anamkomoa mwenzie haaa jamani hii Tanzania kuna vibweka kila kukicha

Ladies, usione mwanamme alikuwa ana muhonga msichana mwenzio ukajua na wewe itakuwa hivyo, kumbuka kila mtu na bahati yake yeye ameitwa Wema na wewe unaitwa Naima

I do the seeking n you do the judging..
 
http://kifltd.files.wordpress.com/2012/01/sintah.jpg

WADADA WALE WENYE TABIA ZA KUVAA NUSU UCHI SASA KUCHAPWA BAKOLA HADHALANI SOMA ZAIDI

$
0
0
 

MKUTANO Mkuu wa Kijiji cha Olgilai wilayani Arumeru umeazimia kuwachapa viboko vijana wa kiume wanaovaa suruali chini ya makalio pamoja na wanawake wanaovaa sketi fupi na suruali zinazobana. Azimio hilo pia limeelekezwa kwa wanafunzi wanaopata mimba au kuozeshwa na kuacha masomo bila sababu za msingi.

Mkutano huo umepitisha maazimio saba yanayolenga kurejesha nidhamu na heshima kijijini Olgilai limefikiwa kutokana na vijana wa kike na kiume kuvaa nguo zisizo na heshima.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Olgilai, Godson Boazi katika barua yake ya Januari 24 mwaka huu kwa viongozi wa makanisa kijijini hapo, aliwaomba kuunga mkono hatua hiyo katika kurekebisha tabia ndani ya jamii yao.

“Viongozi wa dini tunafahamu kazi kubwa ya kutunza kundi la Mungu likae kwenye maadili mema. Hivyo basi tunaomba mtusaidie jukumu hili ambalo tumeambatanisha barua kwenu,”alisema Boaz na kuongeza:



http://3.bp.blogspot.com/-CWtZgweQ57A/UG6t686CSRI/AAAAAAAANao/XGyvHxCs5q8/s1600/frola+mvungi.jpg
 
“Viongozi wa dini tumewaandikia waraka huu tukijua kwamba ninyi ni watu muhimu katika kusaidia jambo hili na kuwafikishia taarifa waumini wenu wote wakubwa kwa wadogo.”

Katika barua yake ambayo MTANZANIA inayo nakala yake Mwenyekiti huyo alisema kwa kauli moja uongozi mkutano huo uliafiki suala hili na kuamuru lianze kutumiwa Januari 24 mwaka huu.

Aliyataja maazimio yaliyopitishwa kuwa ni vijana wanaokaa au kusimama ovyo barabarani na maeneo mengine bila shughuli maalumu watachapwa viboko.

Jingine ni kuwachapa viboko wote watakaovaa nguo zisizofaa katika jamii yao mfano sketi fupi, suruali zilizobana kwa wasichana na akina mama.



 
“Vijana wa kiume wanaovaa suruali zinazojulikana kama mlegezo, uendeshaji ovyo wa pikipiki, wavutaji wa bangi, dawa za kulevya, gongo na wanywaji wa viroba, uchezaji kamari na karata.

“Wanaotukana ovyo barabarani na kupiga kelele za uvunjaji wa amani, wezi wa vitu vikubwa na vidogo kama kuku, ndizi, viazi, mahindi na mboga shambani watashughulikiwa,” alisema Boazi.


Alisema Mkutano Mkuu wa Kijiji ulijiridhisha kuwa matendo hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa nidhamu kijijini hapo na maeneo mengine.
Viewing all 303 articles
Browse latest View live




Latest Images